Haki Mayumba

Muhtasari wa Mpango

Katika SERI, tumepewa ufadhili wa kifedha wa $103,175 kutoka kwa Idara ya U.S. Housing and Urban Development (HUD) ili kusaidia kuangamiza ubaguzi wa makazi kupitia kwa Programu ya Mpango wa Haki Mayumba – Mpango wa Elimu na Msaada (EOI). Mipango yetu itasaidia kuangamiza ubaguzi na chuki katika jumuiya, hivyo kufanya jumuiya yetu mahali ambapo kila mtu anaweza kuishi, kufanya kazi na kuingiliana. Jumuiya zilizo na mapato duni na za watu wachache ziko katika hatari ya ubaguzi wa makazi zaidi kwani zina ufikiaji mdogo zaidi kwa elimu kuhusu haki mayumba, rasilimali na zinaathiriwa zaidi na kulipiza kisasi. Wakati wa COVID-19, mpango wetu unafanyika mtandaoni isipokuwa kutuma baadhi ya barua za moja kwa moja. Kupitia kwa mpango wetu watu hupata rasilimali za elimu kuhusu haki mayumba bila malipo ikiwemo matukio ya kielimu ya bila malipo. Ili kujifunza zaidi na kuhudhuria tukio tafadhali tembelea ukurasa wetu wa kalenda ya haki mayumba. Ili kusaidia wale wanaoamini kuwa wao ni waathiriwa wanaowezekana wa ubaguzi wa makazi tuna simu ya malalamiko wanayoweza kuwasiliana kwayo. Pindi likipokewa, tutakagua lalamiko hilo na kuelekeza lalamiko hilo kwa mshirika wetu ambaye ni wakala wa eneo, Southwest Fair Housing Council (SWFHC). Kisha SWFHC itawasaidia watu walio na madai ya ubaguzi haramu wa makazi kwa kutoa msaada wa upelelezi, ushauri, kupunguza athari ya malalamiko, na kuelekezwa kwa rasilimali ndani ya Arizona.

pexels-photo-3584088
seri-fair-housing-home
seri-fair-housing-moving
seri-fair-housing-contract

Mnamo 1968 Sheria ya Haki Mayumba (FHA) ilitiwa sahihi, na kufanya kuwa kinyume cha sheria kwa watu kubagua katika nyanja yoyote ya makazi kwa kutegemea ukabila, rangi, asili ya kitaifa, dini, kinsia, hali ya kifamilia na ulemavu. FHA hufafanua haya kama kategoria zake saba zinazolindwa na sheria ya shirikisho.

Sheria ya Usawa wa Makazi hutumika wakati watu wanakodisha au kununua nyumba, kuchukua rahani, kutafuta usaidizi wa makazi au kushiriki katika miamala mingine yoyote inayohusiana na makazi.

Ili kuona orodha kamili tafadhali tembelea Ubaguzi wa Makazi Chini ya Sheria ya Haki Mayumba.

 • Kukataa kukodisha, kuuza au kujadiliana kuhusu makazi.
 • Vinginevyo kufanya makazi kutopatikana au kukatisha mtu tamaa ili asinunue au kukodisha nyumba.
 • Kuweka sheria tofauti, masharti au haki za kuuza au kukodisha nyumba.
 • Kutoa haki tofauti au kuzuia haki kwa mtu katika huduma za makazi au nyenzo za nyumba.
 • Kukataa kwa uongo kuwa makazi hayapatikani ili kuangaliwa, kuuzwa au kukodishwa.
 • Kutoa tangazo la nyumba linaloashiria mapendeleo yoyote, uzuiaji au ubaguzi.
 • Kuweka bei tofauti za kuuza au ada za kukodisha kwa kuuza au kukodisha nyumba.
 • Kutumia vigezo tofauti vya kustahiki au matumizi, au viwango vya kuuza au kukodisha au taratibu.
 • Kumsumbua mtu.
 • Kutoa sehemu fulani ya jengo au ujirani kwa mtu.
 • Kukataa kutoa mkopo wa rahani au kutoa usaidizi mwingine wa kifedha kwa ajili ya nyumba.
 • Kukataa kutoa maelezo kuhusu mikopo.
 • Kuweka sheria na masharti tofauti kwa mkopo, kama vile viwango tofauti vya riba, pointi au ada.
 • Tangazo lina kosa. Kuanzia Agosti kodi itaongezeka kwa $50 kila mwezi.”
 • “Huwa tunakubali watu wanaozungumza Kiingereza vyema pekee.”
 • “Unaweza kuwa na starehe zaidi ukiishi mahali pengine. Nitakuonyesha ujirani ulio na misikiti.”
 • “Kwa bahati mbaya, tuna ngazi tu. Hatuwezi kukubali matumizi ya kifaa cha kutembea kwa ajili yako.”
 • “Kuna trafiki nyingi sana katika eneo hili. Si salama kwa watoto kuishi hapa.”
 • “Tunapendekeza wewe na familia yako kukodisha katika ghorofa ya kwanza kwa ufikiaji rahisi.”
 • “Wapenzi ambao ni wataalamu wanapendelewa kwa nyumba hii kutokana na kiwango kikubwa cha kuingia na kuondoka wakati uliopita.”
 • “Kwa bahati mbaya, ukarabati wa choo na vifaa vya kufua haupatikani hadi wiki ijayo.”
 • “Samahani, hiki ni chumba cha mtu mmoja.”
 • “Kutokana na asili yako, tutahitaji kuchukua hati za ziada.”

Jinsi Ya Kuwasilisha Lalamiko Kwa SERI

Iwapo unafikiri umepitia ubaguzi haramu katika makazi unaweza kuwasilisha lalamiko. Tutajibu ndani ya siku 1 ya kazi na kuelekeza lalamiko lako kwa wakala anayefaa. Sisi ni Biashara Inayotumia Mawasiliano ya Relay ya Arizona. Ikiwa unahitaji marekebisho yanayokubalika tafadhali wasiliana nasi.

ADA Accessibility Logo

Fomu ya Mtandaoni
520-306-0938
hotline@seriaz.org
Fomu ya Barua ya Moja kwa Moja

Nyenzo za Mpango

Kwa maswali ya jumla tafadhali wasiliana nasi kupitia kwa 520-321-9488 au seri@seriaz.org.

Kanusho

Nyenzo hii inategemea kazi inayoungwa mkono na Idara ya Makazi na Maendeleo ya Miji (HUD) chini ya Ufadhili wa FHIP EOI FEOI20038 na FEO2100215. Maoni yoyote, utambuzi na mahitimisho au mapendekezo yaliyotolewa katika nyenzo hii ni ya waandishi na sio lazima kuwa yanaakisi mitazamo ya HUD.